Yeremia 4:15
Jeremiah 4:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sauti inatangaza kutoka Dani, ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu.
Jeremiah 4:15 in English
Jeremiah 4:15 · Berean Standard Bible
For a voice resounds from Dan, proclaiming disaster from the hills of Ephraim.
Context
13Tazama! Anakuja kama mawingu,
magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,
farasi wake wana mbio kuliko tai.
Ole wetu! Tunaangamia! 14Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.
Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini? 15Sauti inatangaza kutoka Dani,
ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu. 16“Waambie mataifa jambo hili,
piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu:
‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali,
likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda. 17Wamemzunguka kama watu walindao shamba,
kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.