Yeremia 37:6
Jeremiah 37:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema:
Jeremiah 37:6 in English
Jeremiah 37:6 · Berean Standard Bible
Then the word of the LORD came to Jeremiah the prophet:
Context
4Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. 5Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu. 6Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema: 7“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri. 8Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.