Yeremia 37:5
Jeremiah 37:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu.
Jeremiah 37:5 in English
Jeremiah 37:5 · Berean Standard Bible
Pharaoh’s army had left Egypt, and when the Chaldeans * who were besieging Jerusalem heard the report, they withdrew from Jerusalem.
Context
3Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa Bwana, Mungu wetu.” 4Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. 5Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu. 6Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema: 7“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.