Native Bible

Jeremiah 37:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa Bwana, Mungu wetu.”

Jeremiah 37:3 in English

Jeremiah 37:3 · Berean Standard Bible

Yet King Zedekiah sent Jehucal * son of Shelemiah and Zephaniah the priest, the son of Maaseiah, to Jeremiah the prophet with the message, “Please pray to the LORD our God for us!”

Context

1Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini* mwana wa Yehoyakimu. 2Lakini sio Sedekia, wala watumishi wake, wala watu wa nchi walisikiliza maneno ya Bwana aliyonena kupitia kwa nabii Yeremia. 3Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa Bwana, Mungu wetu.” 4Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. 5Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.