Yeremia 31:4
Jeremiah 31:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakujenga tena nawe utajengeka upya, ewe Bikira Israeli. Utachukua tena matari yako na kwenda kucheza na wenye furaha.
Jeremiah 31:4 in English
Jeremiah 31:4 · Berean Standard Bible
Again I will build you, and you will be rebuilt, O Virgin Israel. Again you will take up your tambourines and go out in joyful dancing.
Context
2Hili ndilo asemalo Bwana:
“Watu watakaopona upanga
watapata upendeleo jangwani;
nitakuja niwape Israeli pumziko.” 3Bwana alitutokea wakati uliopita, akisema:
“Nimekupenda kwa upendo wa milele,
nimekuvuta kwa wema. 4Nitakujenga tena nawe utajengeka upya,
ewe Bikira Israeli.
Utachukua tena matari yako
na kwenda kucheza na wenye furaha. 5Utapanda tena shamba la mizabibu
juu ya vilima vya Samaria,
wakulima watapanda
na kufurahia matunda yake. 6Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele
juu ya vilima vya Efraimu wakisema,
‘Njooni, twendeni juu Sayuni,
kwake Bwana Mungu wetu.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.