Yeremia 31:22
Jeremiah 31:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utatangatanga hata lini, ee binti usiye mwaminifu? Bwana ameumba kitu kipya duniani: mwanamke atamlinda mwanaume.”
Jeremiah 31:22 in English
Jeremiah 31:22 · Berean Standard Bible
How long will you wander, O faithless daughter? For the LORD has created a new thing in the land— a woman will shelter * a man.”
Context
20Je, Efraimu si mwanangu mpendwa,
mtoto ninayependezwa naye?
Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake,
bado ninamkumbuka.
Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku,
nina huruma kubwa kwa ajili yake,”
asema Bwana. 21“Weka alama za barabara,
weka vibao vya kuelekeza.
Zingatia vyema njia kuu,
barabara ile unayoipita.
Rudi, ee Bikira Israeli,
rudi kwenye miji yako. 22Utatangatanga hata lini,
ee binti usiye mwaminifu?
Bwana ameumba kitu kipya duniani:
mwanamke atamlinda mwanaume.” 23Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Bwana akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ 24Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.