Yeremia 31:10
Jeremiah 31:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Sikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni katika nchi za pwani ya mbali: ‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’
Jeremiah 31:10 in English
Jeremiah 31:10 · Berean Standard Bible
Hear, O nations, the word of the LORD, and proclaim it in distant coastlands: “The One who scattered Israel will gather them and keep them as a shepherd keeps his flock.
Context
8Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini
na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia.
Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete,
mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa.
Umati mkubwa wa watu utarudi. 9Watakuja wakilia;
wataomba wakati ninawarudisha.
Nitawaongoza kando ya vijito vya maji
katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa,
kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli,
naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza. 10“Sikieni neno la Bwana, enyi mataifa,
litangazeni katika nchi za pwani ya mbali:
‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya
na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’ 11Kwa kuwa Bwana atamlipia fidia Yakobo
na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao. 12Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni;
watashangilia ukarimu wa Bwana:
nafaka, divai mpya na mafuta,
wana-kondoo wachanga
na ndama wa makundi ya ngʼombe nitakaowapa.
Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri,
wala hawatahuzunika tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.