Yeremia 30:17
Jeremiah 30:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’ asema Bwana, ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’
Jeremiah 30:17 in English
Jeremiah 30:17 · Berean Standard Bible
But I will restore your health and heal your wounds, declares the LORD, because they call you an outcast, Zion, for whom no one cares.”
Context
15Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,
yale maumivu yako yasiyoponyeka?
Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi
nimekufanyia mambo haya. 16“ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa;
adui zako wote watakwenda uhamishoni.
Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara;
wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka. 17Lakini nitakurudishia afya yako
na kuyaponya majeraha yako,’
asema Bwana,
‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa,
Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’ 18“Hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo,
na kuhurumia maskani yake.
Mji utajengwa tena juu ya magofu yake,
nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi. 19Nyimbo za kushukuru zitatoka kwao
na sauti ya furaha.
Nitaiongeza idadi yao
wala hawatapungua,
nitawapa heshima
na hawatadharauliwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.