Yeremia 3:18
Jeremiah 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.
Jeremiah 3:18 in English
Jeremiah 3:18 · Berean Standard Bible
In those days the house of Judah will walk with the house of Israel, and they will come together from the land of the north to the land that I gave to your fathers as an inheritance.
Context
16Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la Bwana,’ ” asema Bwana. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine. 17Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Bwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Bwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. 18Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi. 19“Mimi mwenyewe nilisema,
“ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana
na kuwapa nchi nzuri,
urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’
Nilidhani mngeniita ‘Baba,’
na msingegeuka, mkaacha kunifuata. 20Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,
vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu pia, ee nyumba ya Israeli,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.