Yeremia 25:35
Jeremiah 25:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea.
Jeremiah 25:35 in English
Jeremiah 25:35 · Berean Standard Bible
Flight will evade the shepherds, and escape will elude the leaders of the flock.
Context
33Wakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi. 34Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,
mgaagae mavumbini,
ninyi viongozi wa kundi.
Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;
mtaanguka na kuvunjavunjwa
kama vyombo vizuri vya udongo. 35Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,
viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. 36Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi,
kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao. 37Makao yao ya amani yataharibiwa
kwa sababu ya hasira kali ya Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.