Yeremia 23:21
Jeremiah 23:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mimi sikuwatuma manabii hawa, lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao. Mimi sikusema nao, lakini wametabiri.
Jeremiah 23:21 in English
Jeremiah 23:21 · Berean Standard Bible
I did not send these prophets, yet they have run with their message; I did not speak to them, yet they have prophesied.
Context
19Tazama, dhoruba ya Bwana
itapasuka kwa ghadhabu,
kisulisuli kitazunguka na kuanguka
vichwani vya waovu. 20Hasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.
Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi. 21Mimi sikuwatuma manabii hawa,
lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.
Mimi sikusema nao,
lakini wametabiri. 22Lakini kama wangesimama barazani mwangu,
wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,
nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya
na kutoka matendo yao maovu.” 23“Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”
Bwana asema,
“wala si Mungu aliyeko pia mbali?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.