Yeremia 23:22
Jeremiah 23:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kama wangesimama barazani mwangu, wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya na kutoka matendo yao maovu.”
Jeremiah 23:22 in English
Jeremiah 23:22 · Berean Standard Bible
But if they had stood in My council, they would have proclaimed My words to My people and turned them back from their evil ways and deeds.”
Context
20Hasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.
Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi. 21Mimi sikuwatuma manabii hawa,
lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.
Mimi sikusema nao,
lakini wametabiri. 22Lakini kama wangesimama barazani mwangu,
wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,
nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya
na kutoka matendo yao maovu.” 23“Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”
Bwana asema,
“wala si Mungu aliyeko pia mbali? 24Je, mtu yeyote aweza kujificha
mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”
Bwana asema.
“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”
Bwana asema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.