Yeremia 23:11
Jeremiah 23:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nabii na kuhani wote si wacha Mungu; hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,” asema Bwana.
Jeremiah 23:11 in English
Jeremiah 23:11 · Berean Standard Bible
“For both prophet and priest are ungodly; even in My house I have found their wickedness,” declares the LORD.
Context
9Kuhusu manabii:
Moyo wangu umevunjika ndani yangu;
mifupa yangu yote inatetemeka.
Nimekuwa kama mtu aliyelewa,
kama mtu aliyelemewa na divai,
kwa sababu ya Bwana
na maneno yake matakatifu. 10Nchi imejaa wazinzi;
kwa sababu ya laana, nchi imekauka
na malisho yaliyoko nyikani yamekauka.
Mwenendo wa manabii ni mbaya
na mamlaka yao si ya haki. 11“Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;
hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”
asema Bwana. 12“Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,
watafukuziwa mbali gizani
na huko wataanguka.
Nitaleta maafa juu yao
katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”
asema Bwana. 13“Miongoni mwa manabii wa Samaria
nililiona jambo la kuchukiza:
Walitabiri kwa Baali
na kuwapotosha Israeli watu wangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.