Yeremia 20:14
Jeremiah 20:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ilaaniwe siku niliyozaliwa! Nayo isibarikiwe ile siku mama yangu aliyonizaa!
Jeremiah 20:14 in English
Jeremiah 20:14 · Berean Standard Bible
Cursed be the day I was born! May the day my mother bore me never be blessed.
Context
12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
wewe umjaribuye mwenye haki
na kupima moyo na nia,
hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,
kwa maana kwako
nimeliweka shauri langu. 13Mwimbieni Bwana!
Mpeni Bwana sifa!
Yeye huokoa uhai wa mhitaji
kutoka mikononi mwa waovu. 14Ilaaniwe siku niliyozaliwa!
Nayo isibarikiwe ile siku
mama yangu aliyonizaa! 15Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,
yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,
“Mtoto amezaliwa kwako,
tena mtoto wa kiume!” 16Mtu huyo na awe kama miji ile
ambayo Bwana Mungu
aliiangamiza bila huruma.
Yeye na asikie maombolezo asubuhi
na kilio cha vita adhuhuri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.