Yeremia 2:32
Jeremiah 2:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, mwanamwali husahau vito vyake, au bibi arusi mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu.
Jeremiah 2:32 in English
Jeremiah 2:32 · Berean Standard Bible
Does a maiden forget her jewelry or a bride her wedding sash? Yet My people have forgotten Me for days without number.
Context
30“Nimeadhibu watu wako bure tu,
hawakujirekebisha.
Upanga wako umewala manabii wako
kama simba mwenye njaa. 31“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana:
“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli
au nchi ya giza kuu?
Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,
hatutarudi kwako tena’? 32Je, mwanamwali husahau vito vyake,
au bibi arusi mapambo yake ya arusi?
Lakini watu wangu wamenisahau mimi,
tena kwa siku zisizo na hesabu. 33Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!
Hata wale wanawake wabaya kuliko wote
wanaweza kujifunza kutokana na njia zako. 34Katika nguo zako watu huona
damu ya uhai ya maskini wasio na hatia,
ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.
Lakini katika haya yote
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.