Native Bible

Jeremiah 2:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Nimeadhibu watu wako bure tu, hawakujirekebisha. Upanga wako umewala manabii wako kama simba mwenye njaa.

Jeremiah 2:30 in English

Jeremiah 2:30 · Berean Standard Bible

“I have struck your sons in vain; they accepted no discipline. Your own sword has devoured your prophets like a voracious lion.”

Context

28Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mko katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, ee Yuda. 29“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? Ninyi nyote mmeniasi,” asema Bwana. 30“Nimeadhibu watu wako bure tu, hawakujirekebisha. Upanga wako umewala manabii wako kama simba mwenye njaa. 31“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’? 32Je, mwanamwali husahau vito vyake, au bibi arusi mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.