Yeremia 18:14
Jeremiah 18:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote? Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbali yaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote?
Jeremiah 18:14 in English
Jeremiah 18:14 · Berean Standard Bible
Does the snow of Lebanon ever leave its rocky slopes? Or do its cool waters flowing from a distance ever run dry?
Context
12Lakini wao watajibu, ‘Hakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.’ ” 13Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:
“Ulizia miongoni mwa mataifa:
Ni nani alishasikia jambo kama hili?
Jambo la kutisha sana limefanywa
na Bikira Israeli. 14Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka
kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote?
Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbali
yaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote? 15Lakini watu wangu wamenisahau mimi,
wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu,
zilizowafanya wajikwae katika njia zao
na katika mapito ya zamani.
Zimewafanya wapite kwenye vichochoro
na kwenye barabara ambazo hazikujengwa. 16Nchi yao itaharibiwa,
itakuwa kitu cha kudharauliwa daima;
wote wapitao karibu nayo watashangaa
na kutikisa vichwa vyao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.