Yeremia 17:3
Jeremiah 17:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri na hazina zako zote nitazitoa ziwe nyara, pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia miungu kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote.
Jeremiah 17:3 in English
Jeremiah 17:3 · Berean Standard Bible
O My mountain in the countryside, I will give over your wealth and all your treasures as plunder, because of the sin of your high places, within all your borders.
Context
1“Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma,
imeandikwa kwa ncha ya almasi,
kwenye vibao vya mioyo yao
na kwenye pembe za madhabahu zao. 2Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao
na nguzo za Ashera,*
kandokando ya miti iliyotanda
na juu ya vilima virefu. 3Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri
na hazina zako zote nitazitoa ziwe nyara,
pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia miungu
kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote. 4Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza
urithi niliokupa.
Nitakufanya mtumwa wa adui zako
katika nchi usiyoijua,
kwa kuwa umeiwasha hasira yangu,
nayo itawaka milele.” 5Hili ndilo asemalo Bwana:
“Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu,
ategemeaye mwenye mwili
kwa ajili ya nguvu zake,
ambaye moyo wake
umemwacha Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.