Native Bible

Jeremiah 17:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na nguzo za Ashera,* kandokando ya miti iliyotanda na juu ya vilima virefu.

Jeremiah 17:2 in English

Jeremiah 17:2 · Berean Standard Bible

Even their children remember their altars and Asherah poles by the green trees and on the high hills.

Context

1“Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma, imeandikwa kwa ncha ya almasi, kwenye vibao vya mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zao. 2Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na nguzo za Ashera,* kandokando ya miti iliyotanda na juu ya vilima virefu. 3Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri na hazina zako zote nitazitoa ziwe nyara, pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia miungu kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote. 4Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza urithi niliokupa. Nitakufanya mtumwa wa adui zako katika nchi usiyoijua, kwa kuwa umeiwasha hasira yangu, nayo itawaka milele.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.