Native Bible

Jeremiah 16:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika.

Jeremiah 16:17 in English

Jeremiah 16:17 · Berean Standard Bible

For My eyes are on all their ways. They are not hidden from My face, and their guilt is not concealed from My eyes.

Context

15bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao. 16“Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema Bwana, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba. 17Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika. 18Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.” 19Ee Bwana, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa yatakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo, sanamu zisizofaa kitu ambazo hazikuwafaidia lolote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.