Yeremia 14:9
Jeremiah 14:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache!
Jeremiah 14:9 in English
Jeremiah 14:9 · Berean Standard Bible
Why are You like a man taken by surprise, like a warrior powerless to save? Yet You are among us, O LORD, and we are called by Your name. Do not forsake us!
Context
7Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu,
Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako.
Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa,
nasi tumetenda dhambi dhidi yako. 8Ee Tumaini la Israeli,
Mwokozi wake wakati wa taabu,
kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi,
kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu? 9Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa,
kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa?
Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana,
nasi tunaitwa kwa jina lako;
usituache! 10Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa:
“Wanapenda sana kutangatanga,
hawaizuii miguu yao.
Hivyo Bwana hawakubali;
sasa ataukumbuka uovu wao
na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.” 11Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.