Native Bible

Jeremiah 14:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa.

Jeremiah 14:11 in English

Jeremiah 14:11 · Berean Standard Bible

Then the LORD said to me, “Do not pray for the well-being of this people.

Context

9Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache! 10Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa: “Wanapenda sana kutangatanga, hawaizuii miguu yao. Hivyo Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.” 11Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. 12Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.” 13Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.