Yeremia 14:6
Jeremiah 14:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame na kutweta kama mbweha; macho yao yanakosa nguvu za kuona kwa ajili ya kukosa malisho.”
Jeremiah 14:6 in English
Jeremiah 14:6 · Berean Standard Bible
Wild donkeys stand on barren heights; they pant for air like jackals;* their eyes fail for lack of pasture.”
Context
4Ardhi imepasuka nyufa
kwa sababu hakuna mvua katika nchi;
wakulima wana hofu
na wanafunika vichwa vyao. 5Hata kulungu mashambani
anamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huo
kwa sababu hakuna majani. 6Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame
na kutweta kama mbweha;
macho yao yanakosa nguvu za kuona
kwa ajili ya kukosa malisho.” 7Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu,
Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako.
Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa,
nasi tumetenda dhambi dhidi yako. 8Ee Tumaini la Israeli,
Mwokozi wake wakati wa taabu,
kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi,
kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.