Native Bible

Jeremiah 14:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Yuda anaomboleza, miji yake inayodhoofika; wanaomboleza kwa ajili ya nchi, nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu.

Jeremiah 14:2 in English

Jeremiah 14:2 · Berean Standard Bible

“Judah mourns and her gates languish. Her people wail for the land, and a cry goes up from Jerusalem.

Context

1Hili ndilo neno la Bwana kwa Yeremia kuhusu ukame: 2“Yuda anaomboleza, miji yake inayodhoofika; wanaomboleza kwa ajili ya nchi, nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu. 3Wakuu wanawatuma watumishi wao maji; wanakwenda visimani lakini humo hakuna maji. Wanarudi na vyombo bila maji; wakiwa na hofu na kukata tamaa, wanafunika vichwa vyao. 4Ardhi imepasuka nyufa kwa sababu hakuna mvua katika nchi; wakulima wana hofu na wanafunika vichwa vyao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.