Yeremia 14:3
Jeremiah 14:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakuu wanawatuma watumishi wao maji; wanakwenda visimani lakini humo hakuna maji. Wanarudi na vyombo bila maji; wakiwa na hofu na kukata tamaa, wanafunika vichwa vyao.
Jeremiah 14:3 in English
Jeremiah 14:3 · Berean Standard Bible
The nobles send their servants for water; they go to the cisterns, but find no water; their jars return empty. They are ashamed and humiliated; they cover their heads.
Context
1Hili ndilo neno la Bwana kwa Yeremia kuhusu ukame: 2“Yuda anaomboleza,
miji yake inayodhoofika;
wanaomboleza kwa ajili ya nchi,
nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu. 3Wakuu wanawatuma watumishi wao maji;
wanakwenda visimani
lakini humo hakuna maji.
Wanarudi na vyombo bila maji;
wakiwa na hofu na kukata tamaa,
wanafunika vichwa vyao. 4Ardhi imepasuka nyufa
kwa sababu hakuna mvua katika nchi;
wakulima wana hofu
na wanafunika vichwa vyao. 5Hata kulungu mashambani
anamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huo
kwa sababu hakuna majani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.