Native Bible

Jeremiah 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waambie kwamba hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili,

Jeremiah 11:3 in English

Jeremiah 11:3 · Berean Standard Bible

You must tell them that this is what the LORD, the God of Israel, says: Cursed is the man who does not obey the words of this covenant,

Context

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 2“Sikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu. 3Waambie kwamba hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili, 4maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.’ Nilisema, ‘Nitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 5Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali,’ nchi ambayo mnaimiliki leo.” Nikajibu, “Amen, Bwana.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.