Yeremia 10:3
Jeremiah 10:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, wanakata mti msituni, na fundi anauchonga kwa patasi.
Jeremiah 10:3 in English
Jeremiah 10:3 · Berean Standard Bible
For the customs of the peoples are worthless; they cut down a tree from the forest; it is shaped with a chisel by the hands of a craftsman.
Context
1Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli. 2Hili ndilo asemalo Bwana:
“Usijifunze njia za mataifa
wala usitishwe na ishara katika anga,
ingawa mataifa yanatishwa nazo. 3Kwa maana desturi za mataifa hazina maana,
wanakata mti msituni,
na fundi anauchonga kwa patasi. 4Wanaparemba kwa fedha na dhahabu,
wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike. 5Sanamu zao ni kama sanamu
iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege
nazo haziwezi kuongea;
sharti zibebwe
sababu haziwezi kutembea.
Usiziogope; haziwezi kudhuru,
wala kutenda lolote jema.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.