Waamuzi 8:29
Judges 8:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake.
Judges 8:29 in English
Judges 8:29 · Berean Standard Bible
and he—Jerubbaal * son of Joash—returned home and settled down.
Context
27Gideoni akatengeneza kisibau kwa kutumia ile dhahabu, ambacho alikiweka katika mji wake, yaani, Ofra. Waisraeli wote wakafanya uasherati kwa kukiabudu huko, nacho kikawa mtego kwa Gideoni na jamaa yake. 28Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini. 29Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake. 30Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi. 31Suria wake, aliyekuwa anaishi huko Shekemu, pia alimzalia mwana, ambaye alimwita Abimeleki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.