Native Bible

Judges 8:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini.

Judges 8:28 in English

Judges 8:28 · Berean Standard Bible

In this way Midian was subdued before the Israelites and did not raise its head again. So the land had rest for forty years in the days of Gideon,

Context

26Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilifikia shekeli 1,700,* bila kuhesabu mapambo mengine, pete za masikio na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia zao. 27Gideoni akatengeneza kisibau kwa kutumia ile dhahabu, ambacho alikiweka katika mji wake, yaani, Ofra. Waisraeli wote wakafanya uasherati kwa kukiabudu huko, nacho kikawa mtego kwa Gideoni na jamaa yake. 28Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini. 29Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake. 30Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.