Waamuzi 5:26
Judges 5:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso.
Judges 5:26 in English
Judges 5:26 · Berean Standard Bible
She reached for the tent peg, her right hand for the workman’s hammer. She struck Sisera and crushed his skull; she shattered and pierced his temple.
Context
24“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,
mkewe Heberi, Mkeni,
abarikiwe kuliko wanawake wote
waishio kwenye mahema. 25Aliomba maji, naye akampa maziwa;
kwenye bakuli la heshima
akamletea maziwa mgando. 26Akanyoosha mkono wake
akashika kigingi cha hema,
mkono wake wa kuume
ukashika nyundo ya fundi.
Akampiga Sisera kwa nyundo,
akamponda kichwa chake,
akamvunjavunja na kumtoboa
paji lake la uso. 27Aliinama miguuni pa Yaeli,
akaanguka; akalala hapo.
Pale alipoinama miguuni pake,
alianguka;
pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,
akiwa amekufa. 28“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;
nyuma ya dirisha alilia, akasema,
‘Mbona gari lake linachelewa kufika?
Mbona vishindo vya magari yake
vimechelewa?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.