Waamuzi 5:19
Judges 5:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wafalme walikuja na kufanya vita; wafalme wa Kanaani walipigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido, lakini hawakuchukua fedha wala nyara.
Judges 5:19 in English
Judges 5:19 · Berean Standard Bible
Kings came and fought; then the kings of Canaan fought at Taanach by the waters of Megiddo, but they took no plunder of silver.
Context
17Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani.
Naye Dani, kwa nini alikaa
kwenye merikebu siku nyingi?
Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,
akikaa kwenye ghuba zake ndogo. 18Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,
vilevile nao watu wa Naftali. 19“Wafalme walikuja na kufanya vita;
wafalme wa Kanaani walipigana
huko Taanaki karibu na maji ya Megido,
lakini hawakuchukua fedha wala nyara. 20Kutoka mbinguni nyota zilipigana,
nyota kutoka njia zake
zilipigana na Sisera. 21Mto wa Kishoni uliwasomba,
ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.
Songa mbele, ee nafsi yangu,
kwa ujasiri!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.