Waamuzi 16:24
Judges 16:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema: “Sasa mungu wetu amemtia adui yetu mikononi mwetu, yule aliyeharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.”
Judges 16:24 in English
Judges 16:24 · Berean Standard Bible
And when the people saw him, they praised their god, saying: “Our god has delivered into our hands our enemy who destroyed our land and multiplied our dead.”
Context
22Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. 23Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.” 24Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema:
“Sasa mungu wetu amemtia adui yetu
mikononi mwetu,
yule aliyeharibu nchi yetu
na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.” 25Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa wakasema, “Mleteni Samsoni aje acheze ili tufurahi.” Basi wakamleta Samsoni kutoka mle gerezani naye akacheza mbele yao.
Wakamweka kati ya nguzo mbili. 26Samsoni akamwambia mtumishi aliyeshika mkono wake, “Niweke mahali ambapo ninaweza kuzigusa nguzo ambazo zinategemeza jengo ili nipate kuziegemea.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.