Waamuzi 16:22
Judges 16:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.
Judges 16:22 in English
Judges 16:22 · Berean Standard Bible
However, the hair of his head began to grow back after it had been shaved.
Context
20Yule mwanamke akamwita, “Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!”
Akaamka toka usingizini akasema, “Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakungʼutia mbali na kuwa huru.” Lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha. 21Basi Wafilisti wakamkamata, wakamngʼoa macho yake, wakamchukua wakamteremsha mpaka Gaza. Wakiwa wamemfunga kwa pingu za shaba, wakamweka ili asage ngano huko gerezani. 22Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. 23Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.” 24Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema:
“Sasa mungu wetu amemtia adui yetu
mikononi mwetu,
yule aliyeharibu nchi yetu
na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.