Native Bible

Judges 15:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Samsoni akasema, “Kwa taya la punda malundo juu ya malundo. Kwa taya la punda nimeua watu 1,000.”

Judges 15:16 in English

Judges 15:16 · Berean Standard Bible

Then Samson said: “With the jawbone of a donkey I have piled them into heaps.* With the jawbone of a donkey I have slain a thousand men.”

Context

14Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000. 16Ndipo Samsoni akasema, “Kwa taya la punda malundo juu ya malundo. Kwa taya la punda nimeua watu 1,000.” 17Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi.* 18Kwa kuwa alikuwa amesikia kiu sana, akamlilia Bwana akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.