Native Bible

Judges 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli.

Judges 12:8 in English

Judges 12:8 · Berean Standard Bible

After Jephthah, Ibzan of Bethlehem judged Israel.

Context

6walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo. 7Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi. 8Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. 9Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba. 10Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.