Waamuzi 12:7
Judges 12:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi.
Judges 12:7 in English
Judges 12:7 · Berean Standard Bible
Jephthah judged Israel six years, and when he died, he was buried in one of the cities of Gilead.*
Context
5Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa yeyote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,” 6walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo. 7Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi. 8Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. 9Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.