Native Bible

Judges 10:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini ninyi mmeniacha mimi na kutumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena.

Judges 10:13 in English

Judges 10:13 · Berean Standard Bible

But you have forsaken Me and served other gods, so I will no longer save you.

Context

11Bwana akawaambia, “Wakati Wamisri, Waamori, Waamoni, Wafilisti, 12Wasidoni, Waamaleki na Wamaoni walipowaonea na ninyi mkanililia na kuomba msaada, je, sikuwaokoa kutoka mikononi mwao? 13Lakini ninyi mmeniacha mimi na kutumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena. 14Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!” 15Lakini Waisraeli wakamwambia Bwana, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.