Native Bible

James 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa.

James 1:9 in English

James 1:9 · Berean Standard Bible

The brother in humble circumstances should exult in his high position.

Context

7Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. 8Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote. 9Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa. 10Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani. 11Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.