Native Bible

James 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani.

James 1:10 in English

James 1:10 · Berean Standard Bible

But the one who is rich should exult in his low position, because he will pass away like a flower of the field.

Context

8Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote. 9Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa. 10Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani. 11Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake. 12Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.