Isaya 8:13
Isaiah 8:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu, ndiye peke yake utakayemwogopa, ndiye peke yake utakayemhofu,
Isaiah 8:13 in English
Isaiah 8:13 · Berean Standard Bible
The LORD of Hosts is the One you shall regard as holy. Only He should be feared; only He should be dreaded.
Context
11Bwana alisema nami mkono wake wenye nguvu ukiwa juu yangu, akinionya nisifuate njia za taifa hili. Akasema: 12“Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,
usiogope kile wanachokiogopa,
wala usikihofu. 13Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake
ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,
ndiye peke yake utakayemwogopa,
ndiye peke yake utakayemhofu, 14naye atakuwa mahali patakatifu;
lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa
jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa
na mwamba wa kuwaangusha.
Kwa watu wa Yerusalemu,
atakuwa mtego na tanzi. 15Wengi wao watajikwaa;
wataanguka na kuvunjika,
watategwa na kunaswa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.