Isaya 7:22
Isaiah 7:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali.
Isaiah 7:22 in English
Isaiah 7:22 · Berean Standard Bible
and from the abundance of milk they give, he will eat curds; for all who remain in the land will eat curds and honey.
Context
20Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,* yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 21Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 22Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 23Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,000* za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. 24Watu watakwenda huko wakiwa na upinde na mshale, kwa maana nchi itafunikwa na michongoma na miiba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.