Isaya 7:20
Isaiah 7:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,* yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia.
Isaiah 7:20 in English
Isaiah 7:20 · Berean Standard Bible
On that day the Lord will use a razor hired from beyond the Euphrates *—the king of Assyria—to shave your head and the hair of your legs, and to remove your beard as well.
Context
18Katika siku ile Bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 19Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 20Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,* yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 21Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 22Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.