Native Bible

Isaiah 7:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji.

Isaiah 7:19 in English

Isaiah 7:19 · Berean Standard Bible

And they will all come and settle in the steep ravines and clefts of the rocks, in all the thornbushes and watering holes.

Context

17Bwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.” 18Katika siku ile Bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 19Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 20Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,* yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 21Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.