Isaya 7:21
Isaiah 7:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili.
Isaiah 7:21 in English
Isaiah 7:21 · Berean Standard Bible
On that day a man will raise a young cow and two sheep,
Context
19Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 20Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,* yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 21Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 22Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 23Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,000* za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.