Isaya 65:21
Isaiah 65:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watajenga nyumba na kuishi ndani yake; watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
Isaiah 65:21 in English
Isaiah 65:21 · Berean Standard Bible
They will build houses and dwell in them; they will plant vineyards and eat their fruit.
Context
19Nami nitaifurahia Yerusalemu
na kuwafurahia watu wangu;
sauti ya maombolezo na ya kilio
haitasikika humo tena. 20“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake
mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu,
au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake.
Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja
atahesabiwa kwamba ni kijana tu,
yeye ambaye hatafika miaka mia moja,
atahesabiwa kuwa amelaaniwa. 21Watajenga nyumba na kuishi ndani yake;
watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. 22Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,
au kupanda mazao na wengine wale.
Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,
ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,
wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi
kazi za mikono yao. 23Hawatajitaabisha kwa kazi bure,
wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga,
kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana,
wao na wazao wao pamoja nao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.