Isaya 57:14
Isaiah 57:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tena itasemwa: “Jengeni, jengeni, itengenezeni njia! Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.”
Isaiah 57:14 in English
Isaiah 57:14 · Berean Standard Bible
And it will be said, “Build it up, build it up, prepare the way, take every obstacle out of the way of My people.”
Context
12Nitaifunua haki yako na matendo yako,
nayo hayatakufaidi. 13Utakapolia kwa kuhitaji msaada,
sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe!
Upepo utazipeperusha zote,
pumzi peke yake itazipeperusha,
Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake,
atairithi nchi
na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.” 14Tena itasemwa:
“Jengeni, jengeni, itengenezeni njia!
Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.” 15Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana,
yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu:
“Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu,
lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu
na mwenye roho ya unyenyekevu,
ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu
na kuihuisha mioyo yao waliotubu. 16Sitaendelea kulaumu milele,
wala sitakasirika siku zote,
kwa kuwa roho ya mwanadamu
ingezimia mbele zangu:
yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.