Native Bible

Isaiah 55:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu.

Isaiah 55:6 in English

Isaiah 55:6 · Berean Standard Bible

Seek the LORD while He may be found; call on Him while He is near.

Context

4Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa, kiongozi na jemadari wa mataifa. 5Hakika utaita mataifa usiyoyajua, nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia, kwa sababu ya Bwana Mungu wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekutukuza.” 6Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu. 7Mtu mwovu na aiache njia yake, na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu, arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. 8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.