Isaya 55:8
Isaiah 55:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Bwana.
Isaiah 55:8 in English
Isaiah 55:8 · Berean Standard Bible
“For My thoughts are not your thoughts, neither are your ways My ways,” declares the LORD.
Context
6Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana;
mwiteni maadamu yu karibu. 7Mtu mwovu na aiache njia yake,
na mtu mbaya na ayaache mawazo yake.
Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu,
arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. 8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu,”
asema Bwana. 9“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia,
ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu
na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10Kama vile mvua na theluji
ishukavyo kutoka mbinguni,
nayo hairudi tena huko
bila kunywesha dunia
na kuichipusha na kuistawisha,
hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi
na mkate kwa mlaji,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.