Isaya 54:12
Isaiah 54:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito vingʼaavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
Isaiah 54:12 in English
Isaiah 54:12 · Berean Standard Bible
I will make your pinnacles of rubies, your gates of sparkling jewels, and all your walls of precious stones.
Context
10Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,
hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,
wala agano langu la amani halitaondolewa,”
asema Bwana, mwenye huruma juu yenu. 11“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa,
nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi. 12Nitafanya minara yako ya akiki,
malango yako kwa vito vingʼaavyo,
nazo kuta zako zote za vito vya thamani. 13Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu. 14Kwa haki utathibitika:
Kuonewa kutakuwa mbali nawe;
hutaogopa chochote.
Hofu itakuwa mbali nawe;
haitakukaribia wewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.