Isaya 51:19
Isaiah 51:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Majanga haya mawili yamekuja juu yako: ni nani awezaye kukufariji? Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga: ni nani awezaye kukutuliza?
Isaiah 51:19 in English
Isaiah 51:19 · Berean Standard Bible
These pairs have befallen you: devastation and destruction, famine and sword. Who will grieve for you? Who can comfort you?*
Context
17Amka, amka!
Simama, ee Yerusalemu,
wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Bwana
kikombe cha ghadhabu yake,
wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake,
kikombe kile cha kunywea
kiwafanyacho watu kuyumbayumba. 18Kati ya wana wote aliowazaa
hakuwepo hata mmoja wa kumwongoza,
kati ya wana wote aliowalea
hakuwepo hata mmoja wa kumshika mkono. 19Majanga haya mawili yamekuja juu yako:
ni nani awezaye kukufariji?
Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga:
ni nani awezaye kukutuliza? 20Wana wako wamezimia,
wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara,
kama swala aliyenaswa kwenye wavu.
Wamejazwa na ghadhabu ya Bwana
na makaripio ya Mungu wako. 21Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa,
uliyelewa, lakini si kwa mvinyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.